Vyombo vya habari vya nchini Israel vimeripoti jana jioni kwamba, idadi ya Waisrael waliouawa katika mapigano kati ya Palestina na Israel imezidi 700, huku watu wengine takriban 2,300 wakijeruhiwa, na wengine 100 kutekwa nyara.
Wakati huohuo, Idara ya afya ya Ukanda wa Gaza ya Palestina imesema mashambulizi ya jeshi la Israel kwenye Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 413 na kujeruhi watu 2,300.
Mapigano mapya kati ya Israel na Palestina yalizuka jumamosi baada ya kundi la Hamas kuanza operesheni ya kijeshi dhidi ya Israel, na jeshi la Israel lilijibu mashambulizi hayo kwa kufanya mashambulizi mengi ya anga kwenye Ukanda wa Gaza.
Mpaka ssa mapigano kati ya pande hizo mbili yanaendelea.