Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan yafikia 2,053
2023-10-09 08:30:12| cri

 

Msemaji wa Wizara ya Usimamizi wa Maafa na Masuala ya Kibinadamu ya serikali ya mpito ya Afghanistan Bw. Mullah Janan Shaeq jana amesema, tetemeko la ardhi lililotokea Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo limesababisha vifo vya watu 2,053, na wengine 9,200 kujeruhiwa.

Matetemeko mawili ya ardhi yenye ukubwa wa 6.2 kwenye kipimo cha Richter yalitokea jumamosi iliyopita Kaskazini Magharibi mwa Afghanistan na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.