Rais wa China ampongeza mwenzake wa Fiji kwa kuadhimisha miaka 53 ya uhuru wa nchi hiyo
2023-10-10 14:43:15| cri

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa pongezi kwa njia ya simu kwa mwenzake wa Fiji Wiliame Katonivere kwa kuadhimisha miaka 53 ya uhuru wa nchi hiyo.

Rais Xi amesema, tangu China na Fiji zianzishe uhusiano wa kibalozi, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepata maendeleo makubwa, kunufaisha watu wa nchi mbili, na kuhimiza maendeleo na amani ya kikanda. Ameeleza kuwa anatilia maanani katika kuendeleza uhusiano kati ya China na Fiji, na kupenda kufanya juhudi pamoja na rais Katonivere kuhimiza maendeleo imara ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Fiji.