Mkutano wa 18 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Wafanyakazi cha China wafunguliwa
2023-10-10 21:46:35| CRI

Mkutano wa 18 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Wafanyakazi cha China umefunguliwa Jumatatu asubuhi kwenye Ukumbi Mkuu wa Mikutano ya Umma mjini Beijing.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya juu wa Chama na serikali, akiwemo rais wa China Xi Jinping, Zhao Leji, Wang Huning, Ding Xuexiang na Li Xi, na Cai Qi alitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama.

Mkutano huo umewashirikisha wajumbe 2,000 kutoka nyanja mbalimbali kote nchini China na wawakilishi maalumu zaidi ya 50.