Tanzania mwenyeji wa mkutano wa kupinga ukeketaji
2023-10-10 23:02:20| cri

Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano wa pili wa Kimataifa wa Kutokomeza Ukeketaji ulio chini ya Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Mkutano huu umeanza kufanyika jana Oktoba 09 na kuendelea hadi Oktoba 11, 2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Zaidi ya washiriki 900 wanahudhuria Mkutano huu, kati yao 200 ni washiriki wa ndani na 700 ni kutoka Mataifa mengine.

Kauli mbiu ya Mkutano huu ni“Mabadiliko katika kizazi kimoja kwenda kingine ni muhimu katika kutokomeza vitendo vya ukeketaji”.