Sudan na Iran zarudisha uhusiano wa kidiplomasia


2023-10-10 08:40:54| cri


Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan jana imetangaza kuwa, baada ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia kwa miaka 7, nchi hiyo na Iran zimeamua kurudisha uhusiano huo kati yao.


Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, baada ya mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika miezi kadhaa iliyopita, Sudan na Iran zimekubaliana kukuza uhusiano wa kirafiki kwa msingi wa kuheshimu mamlaka ya kitaifa, usawa, kulinda maslahi ya pamoja na kuishi kwa amani.


Taarifa hiyo pia imesema, nchi hizo mbili zimekubaliana kuongeza ushirikiano ili kuhimiza maslahi ya wananchi wao na kuhakikisha usalama na amani ya kikanda.