Sherehe za uzinduzi wa raundi mpya ya ushirikiano kati ya CMG na vyombo vya habari vya nchi za BRI zafanyika Beijing
2023-10-10 08:38:09| CRI

Wakati kongamano la tatu la kilele cha Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja linakaribia kufanyika, sherehe za uzinduzi wa raundi mpya ya ushirikiano kati ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na vyombo vya habari vya nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja zimefanyika leo Jumatatu mjini Beijing.

Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong alitoa hotuba akisema huu ni mwaka wa 10 tangu rais Xi Jinping wa China atoe pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na dhana ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Kuhimiza ujenzi wa pamoja wa hali ya juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ni hatua halisi ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, pia ni jukwaa muhimu la ushirikiano wa kimataifa na bidhaa ya kimataifa ya umma inayonufaisha dunia. CMG inapenda kufanya kazi na vyombo vya habari vya nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kuchangia nguvu za vyombo vya habari katika kukuza maadili ya pamoja ya binadamu wote, kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kutajirisha na kuendeleza aina mpya za ustaarabu wa binadamu.

"Pendekezo la Pamoja la Kukuza Kufunzana kwa Ustaarabu kati ya CMG na Vyombo vya Habari vya Nchi Zilizojenga kwa Pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja" lilitangazwa kwenye sherehe, na limetoa wito kwa vyombo vya habari kuwa waenezaji wa maadili ya pamoja ya binadamu wote, walinzi wa ustaarabu anuwai wa dunia, na kuongoza mawasiliano na ushirikiano wa kitamaduni.