Israel yazingira miji ya Gaza wakati mapigano na kundi la Hamas yakiendelea
2023-10-10 08:37:05| CRI

Jeshi la Israel limeongeza mashambulio dhidi ya kundi la Hamas na kuzingira kikamilifu miji ya Gaza nchini Palestina katika siku ya tatu ya mapigano kufuatia shambulio la ghafla la Hamas dhidi ya Israel jumamosi iliyopita.

Jana asubuhi, Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel Daniel Hagari aliwaambia wanahabari kuwa, jeshi hilo linashikilia tena jamii zote katika eneo la kusini mwa Israel ambalo lilivamiwa na wapiganaji wa kundi la Hamas jumamosi iliyopita baada ya kuvunja uzio wa usalama kati ya Israel na Gaza.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema, jeshi la nchi hiyo linaongeza usalama katika mpaka wa kaskazini mwa nchi hiyo, ambako wapiganaji kutoka kusini mwa Lebanon wamerusha makombora kuelekea kaskazini mwa Israel jana mchana.