Mkutano wa uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Kenya na mkoa wa Jiangxi wa China wafanyika nchini Kenya
2023-10-11 08:46:13| CRI

Kenya imekuwa mwenyeji wa mkutano wa jukwaa la uwekezaji na biashara la mkoa wa Jiangxi wa nchini China, ambao umehudhuriwa na maofisa wa ngazi ya juu wa nchi hizo mbili, mabalozi, na wawekezaji.

Mkutano huo ulioandaliwa na Shirikisho la Wafanyabiashara na Viwanda la Kenya (KNCCI), umejadili uratibu katika sekta muhimu kama uzalishaji, nishati safi, huduma za afya, utalii, madini na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Mkutano huo wa siku moja ulifanyika chini ya kaulimbiu “Kuboresha ushirikiano wa kirafiki na ustawi wa pamoja” na kusisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Kenya kuendana na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Washiriki wa mkutano huo wametoa wito wa kuanzishwa kwa jukwaa litakalochochea kubadilishana mawazo na kuhamisha teknolojia kati ya wawekezaji wa China na Kenya ili kutimiza manufaa ya pamoja ya kiuchumi na kijamii.