China yachaguliwa tena kuwa mjumbe wa kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa 2024-2026
2023-10-11 11:02:31| cri

China imefanikiwa kwa mfululizo kuwa mjumbe wa kamati ya haki za binadamu ya baraza la awamu ya 78 la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka 2024 hadi 2026. China imetoa shukrani kwa uungaji mkono na uaminifu wa nchi wanachama, huku ikitoa pongezi kwa wajumbe wengine waliochaguliwa.

China inashikilia kuwapa watu kipaumbele, kufuata njia ya maendeleo ya haki za binadamu inayoendana na wakati na kufaa hali ya taifa, kuzidi kuinua kiwango cha uhakikisho wa haki za binadamu na kuhimiza maendeleo ya pande zote ya binadamu katika mchakato wa kuijenga China kuwa nchi ya kisasa. Hii ni mara ya sita kwa China kuwa mjumbe wa kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, ikiwa moja kati ya nchi zinachochaguliwa mara nyingi zaidi kuwa mjumbe wa kamati hiyo. Hii imeonesha kuwa jumuiya ya kimataifa inaridhika na maendeleo ya shughuli ya haki za binadamu nchini China na ushiriki wake katika ushirikiano wa kimataifa wa haki za binadamu .

Kamati ya haki za binadamu imeundwa mwaka 2006, ikiwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhimiza na kulinda haki za binadamu lenye wanachama 47.