Mke wa Rais wa Kenya Rachel Ruto ahimiza kuwepo kwa vazi la taifa
2023-10-11 10:27:46| cri

Mke wa Rais wa Kenya, Mama Rachel Ruto na maafisa wengine wa serikali wapo kwenye juhudi za kuhimiza kuwepo na vazi la taifa.

Wakizungumza katika sherehe za uzinduzi wa Siku ya Utamaduni zilizofanyika jana katika ukumbi wa Bomas, viongozi hao walisema hatua hiyo siyo tu itasaidia kuhifadhi utamaduni wa taifa bali pia kukuza uzalendo.

Mke wa Rais alithibitisha dhamira ya serikali ya kutangaza aina zote za vielelezo vya taifa na kitamaduni vikiwemo fasihi, sanaa, sherehe za jadi, sayansi, mawasiliano, habari, vyombo vya habari, machapisho, maktaba, majengo na aina nyinginezo za urithi wa kiutamaduni. Mama Ruto amesema Siku ya Utamaduni inawapa Wakenya fursa ya kuziba pengo kati ya asili zao mbalimbali.