Watu zaidi ya 1,900 wauawa katika mapigano kati ya Palestina na Israel
2023-10-11 09:29:29| cri


 

Vyombo vya habari vya Israel na mashirika ya matibabu ya Palestina vimesema, mapigano mapya kati ya pande hizo mbili yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,900.

Vyombo vya habari vya Israel jana vilisema, mapigano hayo yamesababisha vifo vya Waisrael zaidi ya 1,008, huku Wizara ya Afya ya nchi hiyo ikisema hospitali mbalimbali nchini humo zimepokea majeruhi 2,901.

Idara ya afya ya Palestina kwenye Ukanda wa Gaza imesema, mashambulizi ya jeshi la Israel dhidi ya Gaza yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 900, na wengine 4,500 kujeruhiwa.