Liberia yapenda kuimarisha uhusiano na China ili kutimiza maendeleo ya pamoja
2023-10-11 08:43:33| CRI

Liberia inapenda kuimarisha uhusiano na China, na kukuza ushirikiano wa kunufaishana ili kutimiza maendeleo ya pamoja.

Rais wa Liberia George Weah amesema hayo alipopokea hati za utambulisho za Balozi mpya wa China nchini humo Yin Chengwu. Rais Weah amesisitiza kuwa Liberia inafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na kuishukuru China kwa msaada wake wa kusaidia maendeleo ya nchi hiyo na kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa upande wake balozi Yin Chengwu amesema, China inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano na Liberia, na inapenda kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili kwa kufuata msingi wa kuheshimiana, kutendeana kwa usawa na kunufaishana. Pia kukuza kuaminiana kisiasa, na kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa pande zote kati ya pande hizo mbili kupata maendeleo mapya.