Viongozi wa Afrika wana matarajio mazuri na mkutano ujao wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
2023-10-12 08:43:43| CRI

 

Mkutano wa 3 wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” utafanyika kuanzia tarehe 17 hadi 18 mjini Beijing, China.

Viongozi wa Afrika wamepongeza mafanikio yaliyopatikana katika miaka 10 iliyopita tangu kutolewa kwa Pendekezo hilo, na kueleza matarajio yao kuhusu mkutano huo.

Rais Denis Sassou-Nguesso wa Jamhuri ya Kongo amesisitiza kuwa ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umewanufaisha watu wa nchi yake, na miundombinu iliyojengwa na kampuni za China imeboresha maisha ya watu kwa kiasi kikubwa.

Naye Waziri wa Fedha wa Ethiopia Ahmad Shide, amepongeza ushirikiano kati ya Ethiopia na China kufuatia Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” katika miaka 10 iliyopita, na kutarajia mkutano huo utaleta fursa nyingi zaidi kwa ushirikiano huo.