Mshauri wa Umoja wa Afrika aonya hatari ya kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Ethiopia
2023-10-12 10:11:30| cri

Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, Bi. Alice Wairimu Nderitu ameonya juu ya kuongezeka kwa hatari ya mauaji ya kimbari na uhalifu unaohusika kufuatia kuongezeka kwa mapigano makali katika mikoa minne nchini Ethiopia.

Bi. Wairimu Nderitu amesema, ana hofu ya kuongezeka kwa hatari ya mauaji ya kimbari katika mikoa ya Afar, Amhara, Oromia na Tigray kufuatia ripoti za kuendelea kwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo katika maeneo hayo.

Ametolea mfano ripoti za wapiganaji kuua familia nzima na kulazimisha ndugu wa karibu kushuhudia mauaji hayo dhidi ya wapendwa wao, huku jamii nzima zikikimbia makazi yao ama kulazimishwa kuondoka kwenye nyumba zao.