Maelfu ya Watu wauawa katika mapigano kati ya Palestina na Israel
2023-10-12 14:38:17| cri


Vyombo vya habari vya Israel pamoja na jeshi la nchi hiyo na Wizara ya Afya ya Palestina zimesema, watu 2,200 wameuawa na wengine zaidi ya 8,000 kujeruhiwa tangu kutokea kwa mapigano mapya kati ya Palestina na Israel.

Jeshi la Israel jana limesema, mapigano hayo yamesababisha vifo vya Waisrael 1,200, na kundi la Hamas limerusha makombora 4,500 kwa Israel.

Wizara ya Afya ya Palestina nayo imesema, Wapalestina 1,078 wameuawa kwenye Ukanda ya Gaza na kando ya magharibi ya Mto wa Jordan kufuatia mapigano hayo.