Tanzania kufanya mageuzi kiuchumi
2023-10-12 10:12:04| cri

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema nchi hiyo ni moja ya nchi za Afrika zinazofanya mageuzi makubwa kiuchumi kwenye sera na sheria zake ili kuvutia zaidi mitaji kutoka nje ya nchi.

Rais Samia amesema hayo alipohutubia Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na India lililofanyika jijini New Delhi, ambapo katika mkutano huo, Rais Samia pia alishuhudia kubadilishana kwa hati za makubaliano baina ya Tanzania na India.

Pia Rais Samia amesema, India ina kila sababu ya kuongoza katika uwekezaji nchini Tanzania, kutokana na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na historia inayoziunganisha.