Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja laleta matarajio mapya ya maendeleo barani Afrika
2023-10-12 08:47:15| cri

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Nigeria inayoshughulikia Uhusiano wa Nigeria na China, Bw. Jafaru Yakubu amesema, ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja umepata matokeo mazuri. Amesema ana imani kuwa, chini ya uhamasishaji wa ujenzi wa pamoja wa Pendekezo hilo, ushirikiano kati ya nchi za Afrika na China utaleta matarajio mapya ya maendeleo kwa nchi za Afrika. .

Bw. Yakubu amesema, miradi ya kujikimu iliyojengwa kwa pamoja kati ya Nigeria na China imewanufaisha sana wenyeji na pia imechangia kukuza mchakato wa ukuaji wa miji na uchumi wa Nigeria, na maendeleo ya kijamii.