Huawei yaahidi kuendeleza ujumuishi wa kidijitali nchini Kenya kwa kupitia teknolojia za uvumbuzi
2023-10-12 08:44:25| CRI


 

Kampuni ya mawasiliano ya China, Huawei, imeahidi kuisaidia Kenya kuongeza kasi yake ya ujumuishi wa kidijitali, na kuhakikisha kupanua upatikanaji wa majukwaa na huduma za moja kwa moja mtandaoni kwa kutoa teknolojia za kiuvumbuzi.

Ofisa mkuu wa teknolojia wa Ofisi ya Huawei kanda ya Kusini mwa Afrika, Tony Li, amesema hayo katika mkutano wa kikanda uliofanyika mjini Nairobi, Kenya. Amesema nchi hiyo tayari imeshuhudia maendeleo dhahiri katika muongo uliopita, kwa kuanza kutumia mitandao ya 4G na 5G.

Amesema teknolojia ni msingi unaoruhusu kila mjasiriamali kufungua biashara, kila mwalimu kuwafundisha wanafunzi bila kujali sehemu waliyoko duniani, na kila mwananchi kupata huduma bora za afya.