Umoja wa Afrika na IOM zazindua pendekezo la kuboresha usimamizi wa uhamiaji barani Afrika
2023-10-12 08:45:00| CRI


 

Pendekezo jipya linaloitwa Africa Diplomatic Indaba (ADi) limezinduliwa ili kuboresha usimamizi wa uhamiaji na uhamaji wa wataalamu barani Afrika.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika jana imesema, Pendekezo hilo limezinduliwa na Kamati ya Umoja huo kwa kushirikiana na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), nchi za Afrika, mashirika ya kiuchumi ya kikanda na wenzi wengine.

Taarifa hiyo imesema, Pendekezo hilo linalenga kuunganisha wanachama wa kidiplomasua na wabunge na viongozi kwa ajili ya majadiliano ya pamoja ya kuboresha usimamizi wa uhamiaji na uhamaji wa wataalamu barani Afrika.

Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Monique Nsazabaganwa amesema kwenye uzinduzi huo, kuwa pendekezo hilo litasaidia kuboresha nafasi ya Afrika kuhusu uhamiaji na uhamaji wa wataalamu.