Umoja wa Mataifa watoa fedha ili kukabiliana na mafuriko nchini Somalia
2023-10-12 08:45:40| CRI


 

Umoja wa Mataifa umetoa dola za kimarekani milioni 15 ili kusaidia kukabiliana na athari zitakazotokana na mvua za El Nino nchini Somalia.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, fedha hizo zinalenga maeneo yaliyo hatarini zaidi kukumbwa na mafuriko yaliyoko mikoa ya Hirshabelle na Jubaland kutokana na kufurika kwa mito. Pia Ofisi hiyo imesema, wasiwasi zaidi ni kutokea kwa mafuriko ya ghafla katika maeneo ya mijini ambako wakimbizi wa ndani wanaishi.

Kwa upande mwingine, OCHA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuongeza maeneo ya malisho ya mifugo na maji, na pia upatikanaji wa maziwa, jambo litakalosaidia familia kukabiliana na mahitaji yao ya chakula.