Jukwaa la 11 la vyombo vya habari vya video duniani lafanyika Beijing
2023-10-12 23:10:47| cri

Jukwaa la 11 la vyombo vya habari vya video duniani, lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, limefanyika leo Oktoba 12 hapa Beijing. Naibu mkurugenzi wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkuu wa CMG, Bw. Shen Haixiong na mkurugenzi wa ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China Bw. Sun Yeli wamehudhuria na kuhutubia jukwaa hilo.

Kwenye hotuba yake, Bw. Shen Haixiong amesema, ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja umeleta pamoja dunia nzima iwe karibu zaidi. CMG ni mshiriki, shuhuda na mfafanuzi wa pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja. Kwa mujibu wa mwongozo wa Rais Xi Jinping, CMG imekuwa inachangia ujenzi wa Ukanda Moja, Njia Moja kwa njia ya utoaji wa habari na ushirikiano wa kimataifa kupitia kuunganisha fikra, sanaa na teknolojia. Amesema, CMG inapenda kushirikiana na vyombo vya habari vya kimataifa, kubeba majukumu ya wanahabari na kuendeleza urafiki wa Njia ya Hariri, na kutoa nguvu ya vyombo vya habari kwenye ukurasa mpya wa ujenzi wa Ukanda Moja, Njia Moja.

Ofisa mtendaji mkuu wa Muungano wa Radio Afrika Gregoire Ndjaka, mkurugenzi mkuu wa shirika la habari la Umoja wa Falme za Kiarabu Mohamed Jalal Alrayssi, mwenyekiti wa Muungano wa Habari wa Nchi za Visiwa vya Pasifiki Kora Nou, katibu mkuu wa Muungano wa Radio wa Asia-Pasifiki Ahmed Nadeem, maneja mkuu wa Muungano wa Mabadilishano ya Habari wa Ulaya Adrian Wells na mhariri mtendaji mkuu wa gazeti la Lianhe Zaobao la Singapore Han Yong May wametoa hotuba kwenye jukwaa hilo.