Mjumbe maalumu wa China azungumza na naibu mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel
2023-10-13 10:36:41| cri

Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia suala la Mashariki ya Kati Bw. Zhai Jun tarehe 12 alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na naibu mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel anayeshughulikia mambo ya Asia na Pasifiki Bw. Rafi Harpaz juu ya hali ya Israel na Palestina.

Zhai Jun alisema China inafuatilia hali ya wasiwasi kati ya Israel na Palestina na hali ya kuibuka kwa mvutano. China inatoa wito wa kusimamisha mvutano haraka iwezekanavyo, kurejesha mazungumzo ya amani chini ya msingi wa “Mpango wa nchi mbili”, na kuzidisha imani ya watu wa pande mbili juu ya kutimiza amani. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya kazi ya kiutendaji, na kuepuka kuchochea zaidi hali ya wasiwasi na kusababisha janga la kibinadamu. China inatarajia kwa moyo wa dhati kuwa Israel na Palestina zitaishi kwa amani.

Kwa upande wa Israel, Harpaz alieleza maoni na msimamo wa Israel juu ya hali ya sasa ya Israel na Palestina, na kusema Israel itawalinda raia wa China walioko nchini humo kadri iwezekanavyo.