Umoja wa Mataifa wachunguza vitendo visiyofaa vilivyofanywa na walinda amani nchini DRC
2023-10-13 08:56:09| CRI

Umoja wa Mataifa unachukua hatua dhidi ya vitendo visivyofaa vilivyofanywa na askari wake wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja huo Stephane Dujarric amesema, Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRC imechukua hatua kali ikiwa ni kujibu ripoti za vitendo visivyostahili vinavyofanywa na walinda amani wa Tume hiyo, ikiwemo uhalifu wa kingono na udhalilishaji.

Ingawa Msemaji huo hakuweka wazi nchi ambayo askari wanaofanya vitendo hivyo wanatokea, kulikuwa na ripoti zilizotolewa zinadai kuwa, askari wanaofanya vitendo hivyo wanatoka nchini Afrika Kusini.