Kenya yasema watu milioni 2.8 bado wanahitaji msaada wa chakula
2023-10-13 08:56:13| cri


 


Ripoti iliyotolewa jana na Mamlaka ya Kitaifa ya Udhibiti wa Ukame ya Kenya (NDMA) imesema, kutokana na hali ya ukame inayoendelea, wakenya milioni 2.8 katika maeneo kame na nusu kame bado wanahitaji msaada wa chakula . 


NDMA imesema idadi kubwa ya watu walioathirika wako katika kaunti 23, kati yao kaunti 18 ziko kwenye hali ya ukame wa kawaida wa mpito, huku nyingine 5 ziko kwenye hali ya tahadhari na zinahitaji ufuatiliaji wa karibu.


Ripoti hiyo imesema, hali ya utapiamlo ni matokeo ya majira ya uhaba wa mvua katika misimu iliyopita, hivyo maisha bado yako katika hali ya kurejea upya.