China yaendelea kuchukua jukumu kubwa katika kufikia maendeleo ya amani barani Afrika
2023-10-13 08:55:19| cri

Mwakilishi wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Zhang Jun jana amesema, China itaendelea kutoa mchango katika maendeleo ya amani barani Afrika na kuongeza ushirikiano kati ya Afrika na jumuiya ya kimataifa.

Balozi Zhang amesema, katika miaka ya hivi karibuni, Umoja wa Afrika na mashirika ya kikanda yamekabiliana kikamilifu na changamoto za amani na usalama, na kuhimiza kutumia njia za Afrika kutatua matatizo ya Afrika.

Balozi Zhang pia amesema, China siku zote imekuwa ikiunga mkono ujenzi wa uwezo wa Afrika kama sehemu muhimu ya ushirikiano wake na Afrika, na imejikita kuisaidia Afrika kutimiza utandawazi wa uchumi na mambo ya kisasa na kupata maendeleo endelevu.