Rais wa Guinea ya Ikweta atoa wito wa Umoja wa Afrika ili kupambana na ukoloni mamboleo
2023-10-13 08:57:27| CRI

Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema ametoa wito kwa nchi za Afrika kuchukua hatua za pamoja katika kupambana dhidi ya ukoloni mamboleo.

Katika hotuba yake kwa taifa wakati wa kumbukumbu ya miaka 55 tangu nchi hiyo ipate uhuru, rais Nguema amesema kutokana na uhusiano kati ya nchi za Afrika na watawala wake kuendelea kuwa na mtindo wa ukoloni mamboleo, Guinea ya Ikweta na nchi zote za Afrika zinapaswa kuchukua hatua za pamoja na kuchukua uwajibikaji wa masuala yao yenyewe, bila ya kuingiliwa na nguvu za nje.

Rais Nguema amewakosoa baadhi watu wasio wazalendo wanaoendelea kula njama na baadhi ya nchi na mashirika ya kimataifa ili kubadili mfumo wa kisiasa wa nchi zao kwa kutumia mabavu.