Jeshi la Israel lajiandaa kufanya mashambulizi ya ardhini, baharini na angani dhidi ya ukanda wa Gaza
2023-10-16 08:37:16| CRI

Jeshi la ulinzi la Israel limesema linapanga kuongeza mashambulizi ambayo yatajumuisha mashambulizi kutoka ardhini, baharini na angani dhidi ya kundi la Hamas la nchini Palestina.

Jeshi hilo limesema kuwa wanajeshi wake wamepelekwa katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo ili kuongeza utayari wa operesheni kwa hatua zinazofuata za kijeshi zitakazozingatia zaidi operesheni ya ardhini.

Wakati huohuo, Wizara ya Afya ya Palestina imesema jana kuwa, hadi kufikia saa tatu asubuhi jana jumapili, mapigano mapya kati ya Palestina na Israel yalisababisha vifo vya watu 2,329 na wengine 9,042 kujeruhiwa katika Ukanda wa Gaza.