Utawala bora unahitaji kutoa kipaumbele kwa ustawi wa watu
2023-10-16 10:58:08| CRI

Itikadi ya maendeleo inayozingatia zaidi watu sio dhana ya kufikirika tu au isiyoeleweka. Haipaswi kubaki kuwa kauli ya mdomo tu au kuwa wazo tu, bali inapaswa kuonekana kwenye nyanja zote za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Ni lazima tuimarishe ubwana wa watu, tuitikie matarajio ya watu kuwa na maisha bora, tutambue, tulinde na kuendeleza maslahi ya kimsingi ya umma. Tunapaswa kuhakikisha kuwa maendeleo ni ya watu, yanawategemea watu, na yanawanufaisha wananchi yakiwa ni mafanikio ya pamoja.