Rais wa Uganda aonya mashambulio ya kulipiza kisasi kufuatia shambulio la anga dhidi ya kambi za kundi la ADF nchini DRC
2023-10-16 09:06:07| CRI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameonya juu ya mashambulio ya kulipiza kisasi ya waasi wa kundi la ADF kufuatia mashambulio ya anga dhidi ya kambi za kundi hilo zilizoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidekomkrasia ya Kongo (DRC).

Katika taarifa yake, rais Museveni amesema, jumamosi iliyopita, ndege za kivita za kijeshi zilifanya shambulio la pili la anga kwenye maficho ya waasi wa ADF katika maeneo manne tofauti ya mpaka wa magharibi upande wa Bundibugyo-Semiliki, na kusababisha vifo vya wapiganaji kadhaa wa kundi hilo.

Amesema matokeo ya mashambulio hayo ni kwamba, waasi wa ADF wanaingia tena nchini Uganda kutokea DRC, na kujaribu kufanya vitendo vya kigaidi nchini humo.

Tangu mwaka 2022, vikosi vya jeshi la Uganda na Jeshi la DRC wamekuwa wakipambana kwa pamoja na kundi la waasi la ADF.