Watu 28 wafariki katika ajali ya boti DRC
2023-10-16 08:23:28| CRI

Watu 28 wamefariki na wengine 261 hawajulikani walipo baada ya boti waliyopanda kuzama katika Mkoa wa Equateur, kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ijumaa iliyopita.

Naibu gavana wa Jimbo la Equateur Bw. Taylor Ng’anzi, amewaambia wanahabari kuwa, ijumaa usiku, boti hiyo iliyokuwa imebeba abiria wengi kuliko inavyotakiwa, ilizama kwenye maji ya Mto Kongo katika Mkoa wa Equateur.

Idara husika zimeanza kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuwawajibisha wahusika wa ajali hiyo.