CMG na vyombo vya habari vya Afrika watoa kwa pamoja Pendekezo la Utekelezaji la Ukanda Moja, Njia Moja
2023-10-16 08:52:01| CRI

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na vyombo vya habari vya Afrika vimetoa kwa pamoja Pendekezo la Utekelezaji la Ukanda Mmoja, Njia Moja kwa Vyombo vya Habari vya China na Afrika, ambalo limeungwa mkono na vyombo vya habari na taasisi 50 za Afrika.

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amesema, mwaka huu ni wa kumi tangu Rais wa China Xi Jinping alipotoa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na katika muongo uliopita, ushirikiano kati ya China na Afrika umeonesha uhai mkubwa na uko mbioni kujenga jumuiya ya kiwango cha juu yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika. Amesema CMG inapenda kubadilishana maoni na wenzake wa Afrika, na kushirikiana nao bega kwa bega katika kuelezea urafiki na ushirikiano kati ya pande hizo na matunda mengi yaliyopatikana kwenye ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja linatarajiwa kufunguliwa kesho jumanne hapa Beijing.