Rais wa China akutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia
2023-10-17 14:38:21| cri

Rais wa China Xi Jinping leo hapa Beijing, amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ambaye yuko nchini China kuhudhuria Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na pia kufanya ziara rasmi nchini humo.

Viongozi hao wametoa taarifa ya pamoja kuhusu kuanzisha uhusiano wa kimkakati wa siku zote.

Rais Xi amesema, katika muongo mmoja uliopita, ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kati ya China na Ethiopia umepewa umuhimu mkubwa katika ushirikiano wa China na Afrika.

Amesema nchi hizo mbili zinapaswa kuchukulia kuanzishwa kwa uhusiano wa kimkakati wa siku zote kama fursa ya kuendeleza maendeleo ya pamoja na ushirikiano wa kunufaishana, kuboresha mshikamano na ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kulinda usawa na haki ya kimataifa.