Zaidi ya wanafunzi 100 waugua katika shule ya Amabuko huko Kisii
2023-10-17 14:31:57| cri

Zaidi ya wanafunzi 100 katika shule ya sekondari Mchanganyiko ya Amabuko iliyoko Keroka, Kisii wamelazwa hospitalini baada ya kuugua.

Wanafunzi hao wanalalamika kuwa na maumivu makali ya tumbo na kuharisha. Sababu bado haijajulikana, lakini mwalimu mkuu Rawlings Juma anasema wanajaribu kudhibiti hali hiyo. Wanafunzi hao wamelazwa katika Hospitali ya St Catherine Ichuni, Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Keroka, Hospitali ya Gucha na Hospitali ya Kufundishia na Rufaa ya Kisii (KTRH).

Afisa Mkuu Mtendaji wa KTRH Dkt Oimeke Mariita alithibitisha kwamba wamepokea baadhi ya wanafunzi kutoka shuleni kwa ajili ya matibabu.