Tanzania yapitia sera ya TEHAMA ili kuunga mkono uchumi wa kidijitali
2023-10-17 09:53:01| CRI

Serikali ya Tanzania imeanza kupitia sera yake kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano TEHEMA, ili kuiwezesha kuunga mkono uchumi wa kidijitali unaolenga kuleta mabadiliko kwenye uchumi wa nchi hiyo.

Naibu katibu wa kudumu wa wizara ya habari na TEHAMA Bw. Celestine Kalele amesema marekebisho ya sera ya TEHAMA ya Tanzania yanakusudia kujenga mazingira mwafaka ya kukuza uchumi wa kidijitali.

Bw. Kalele amesema hayo katika mkutano wa 7 wa TEHAMA uliofanyika Dar es Salaam, huku akiongeza kuwa serikali itaendelea kujenga mazingira mwafaka yanayowawezesha wawekezaji kufanya uvumbuzi wakati nchi hiyo ikipiga hatua kutumia teknolojia hiyo katika kuhimiza uchumi wa kidijitali.

Pia amesema wanawake na wasichana wanatakiwa kutumia majukwaa ya TEHAMA yanayopatikana kwa shughuli zao za kila siku ili kuwawezesha kiuchumi.