Kitabu cha rais wa China Xi Jinping kinachozungumzia kwa undani Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kimechapishwa kwa lugha za Kiarabu, Kihispania, Kireno na Kijapani.
Hafla ya uzinduzi wa matoleo hayo iliyoandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China na Kundi la Mawasiliano ya Kimataifa la China ilifanyika jana jumatatu na kuhudhuriwa na Zaidi ya watu 100, wakiwemo wajumbe wa nchi zilizojiunga na BRI, wataalamu, wasomi, na wajumbe wa sekta ya ukalimali na uchapishaji.
Ikiwa ni miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, watu walioshiriki kwenye hafla hiyo wamesema, katika muongo mmoja uliopita, ushirikiano wa Pendekezo hilo kutoka kutolewa kwake na China hadi utekelezaji wake duniani, kutoa wazo mpaka vitendo halisi, na kutoka nadharia mpaka uhalisia, BRI imepata mafanikio makubwa yanayoonekana kidhahiri.