Kampuni ya MOJA Expressway inayosimamia ukusanyaji wa ushuru kwenye barabara ya Nairobi Expressway iliyojengwa na kampuni ya China nchini Kenya, imeibuka mshindi kwenye vipengele viwili vya Tuzo za Afrika Mashariki za Usafiri 2023.
Mfumo wa ukusanyaji ushuru wa kielektroniki wa barabara (ETC) wa barabara hiyo umenyakua tuzo ya "Uvumbuzi bora wa kiteknolojia kwenye usafiri", na pia umepata tuzo ya "Usafiri Endelevu".
Mfumo wa ETC ni ubunifu unaowawezesha madereva kulipa ushuru wa barabara kwenye njia hiyo kwa urahisi na kuokoa muda. Madereva na magari yao wanatakiwa kujiandikishwa kwanza, kisha chip huwekwa kwenye gari, na kuwaruhusu kuweka pesa kwenye chip kwa ajili ya huduma hiyo. Mfumo huo umepongezwa na madereva wa Kenya.