Kenya yazindua vigezo ili kuhimiza usalama wa chakula
2023-10-17 08:43:14| CRI

Kenya jana Jumatatu ilizindua vigezo 37 vitakavyoielekeza sekta ya kilimo kuhimiza usalama wa chakula.

Waziri wa Biashara, Uwekezaji na Viwanda wa Kenya Bibi Rebecca Miano amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa vigezo hivyo vilivyoidhinishwa vinahusisha aina nyingi za chakula, ikiwemo sukari, kuku, chai, nyama, pilipili, mchele, maziwa na bidhaa za ngano.

Akiongea kwenye maadhimisho ya Siku ya Vigezo Duniani, waziri huyo amesema vigezo hivyo vitahakikisha familia za Kenya zitatumia tu chakula kinachofaa kutumiwa na binadamu.