Ofisa mwandamizi wa China akutana na rais wa Kenya
2023-10-17 09:13:51| CRI

Ofisa mwandamizi wa China Bw. Li Xi jana Jumatatu alikutana na rais wa Kenya William Ruto aliyewasili China kuhudhuria Mkutano wa tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa “ Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Bw. Li Xi ambaye ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amesema China iko tayari kuhimiza kazi ya kuunganisha pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRI) na mkakati wa maendeleo wa Kenya, na kufanya juhudi kupata mafanikio katika uhusiano wenzi wa kimkakati wa pande zote na Kenya.

Rais Ruto amesema BRI imeleta manufaa yanayoonekana kwa watu wa Kenya na China, na pia ameeleza matumaini yake ya kuinua uhusiano wa nchi hizo mbili hadi kiwango kipya.