Uganda na DRC zakubaliana kuondoa ada ya visa ili kuboresha mawasiliano
2023-10-17 14:32:40| cri

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimekubaliana kuondoa ada ya visa kwa wananchi wanaosafiri kati ya nchi hizo jirani.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema, uamuzi huo umefikiwa wakati wa mkutano wa 8 wa kawaida wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Uganda na DRC uliofanyika mjini Kinshasa.

Taarifa hiyo imesema, pande hizo mbili pia zimejadili masuala yanayohusu ushirikiano wa kijeshi na usalama, kuhakikisha usalama na mipaka ya pamoja, kuondoa makundi yenye silaha, na kupambana dhidi ya ueneaji wa silaha haramu.