Rais Ruto asema Ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” wahimiza ushirikiano kati ya Kenya na China
2023-10-18 09:32:02| CRI

Rais William Ruto wa Kenya amesema kupitia ujenzi wa pamoja wa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, China na Kenya zimeimarisha ushirikiano wa pande mbili, na kujenga mazingira mazuri zaidi ya urafiki na ushirikiano.

Rais Ruto amesema ziara yake hapa China ya kuhudhuria Mkutano wa Baraza la tatu la Ushirikiano wa Kimataifa la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” inalenga kusherehekea mafanikio yaliyopatikana katika miaka kumi iliyopita ya “Ukanda Moja na Njia Moja”, kupeana uzoefu na kujadili kuhusu namna ya kufanya vizuri zaidi katika siku za baadaye, hasa katika sekta ya teknolojia ya kidijitali.

Pia amesema katika miaka kumi iliyopita, kumekuwa na mafanikio halisi yenye ufanisi katika ujenzi wa pamoja na “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, huku akiongeza kuwa wamejenga daraja la ushirikiano kati ya China na Afrika.