Rais wa China atangaza hatua nane kuunga mkono ushirikiano wa ubora wa juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja
2023-10-18 14:33:44| cri

Rais wa China Xi Jinping, leo ametangaza hatua nane kubwa ambazo China itazichukua ili kuunga mkono ushirikiano wa ubora wa juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Hatua ya kwanza ni kwamba China itajenga mtandao wa muunganiko wa pande nyingi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja. Amesema China itaongeza kasi ya maendeleo ya reli ya kasi ya China na Ulaya, kushiriki katika ushoroba wa kimataifa wa usafiri wa Caspian, na kuwa mwenyeji wa Kongamano la Ushirikiano wa Kimataifa wa Reli ya Kasi ya China na Ulaya.

Hatua ya Pili iliyotangazwa na rais Xi ni kuwa China itaunga mkono uchumi wa wazi wa dunia, wakati thamani ya jumla ya bidhaa na huduma ikitarajiwa kuvuka dola za kimarekani trilioni 32 na dola trilioni 5 za kimarekani mtawalia katika kipindi cha mwaka 2024 mpaka 2028.

Tatu, rais Xi amesema China itafanya ushirikiano wa kivitendo katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kuahidi kutoa ufadhili zaidi wa kifedha kusaidia miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja katika msingi wa operesheni za soko na biashara.

Hatua ya nne iliyotangazwa na rais wa China ni kwamba nchi hiyo itaendelea kuboresha maendelo ya kijani, na kwamba China itaongeza ushirikiano wa kina katika maeneo kama miundombinu ya kijani, nishati ya kijani na usafiri wa kijani, na kuunga mkono Muungano wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kijani wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Hatua ya Tano iliyotangazwa na rais Xi ni kwamba, China itaendelea kuendeleza uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, na pia itaendelea kutekeleza Mpango Kazi wa Uvumbuzi wa Sayansi na Teknolojia wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Rais Xi ameitaja hatua ya Sita kuwa China itaunga mkono mawasiliano ya watu kwa watu, ambapo nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Liangzhu kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kuhusu ustaarabu na nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Hatua ya Saba aliyotangaza rais Xi ni kwamba China itaboresha ushirikiano wenye msingi wa uaminifu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Rais Xi ameitaja hatua ya Nane na ya mwisho, kuwa China itaimarisha ujenzi wa taasisi kwa ajili ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja. Amesena China itafanya kazi na nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja kuimarisha ujenzi wa majukwaa ya ushirikiano ya pande nyingi katika maeneo mengi ikiwemo nishati, ushuru, fedha, maendeleo ya kijani, kupunguza majanga, kupambana na ufisadi, vyombo vya habari na maeneo mengine.