Rais Xi apendekeza kuhimiza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kwa njia ya udhati
2023-10-18 12:46:07| cri

Rais Xi Jinping wa China amependekeza kuhimiza ushirikiano wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kwa njia ya udhati.

Xi ameyasema hayo katika hotuba yake muhimu kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Rais Xi ametangaza kuwa pamoja na washirika wake wa ushirikiano, China itatoa Mafanikio na Matarajio ya Ujenzi wa Udhati wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Kanuni za Ngazi ya Juu za Ujenzi wa Udhati wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kuanzisha Mfumo wa Tathmini ya Udhati na Uzingatiaji wa Makampuni Yanayohusika katika Ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja. Pia China itashirikiana na mashirika ya kimataifa kufanya utafiti na mafunzo ya kukuza udhati katika ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Aidha China itaendelea kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kushirikiana na washirika wa BRI kuimarisha ujenzi wa majukwaa ya ushirikiano wa pande nyingi.