Rais wa China asema binadamu ni jamii yenye hatma ya pamoja
2023-10-18 11:27:14| cri

Rais wa China Xi Jinping amesema, binadamu ni jamii yenye hatma ya pamoja.

Akizungumza leo hapa Beijing, rais Xi amesema China inaweza kufanikiwa pale dunia nzima inapofanikiwa, na kwamba China inapofanya vizuri, dunia itakuwa nzuri Zaidi.

Rais Xi amesema, kupitia ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, China inafungua mlango wake Zaidi kwa dunia, huku mikoa yake ikibadilika kutoka kuwa ya nyuma hadi kusonga mbele, na maeneo ya pwani yakipanda ngazi mpya katika ufunguaji wa mlango.

Amesema China imekuwa mwenzi muhimu wa biashara kwa Zaidi ya nchi na sehemu 140 duniani, na ni moja ya chanzo kikuu cha uwekezaji kwa nchi nyingi Zaidi. Ameongeza kuwa, uwekezaji wa China kwa nchi za nje na uwekezaji wa kigeni nchini China vyote vimeboresha urafiki, ushirikiano, hali ya kuaminiana na matumaini.