Xi asema ushirikiano wa kunufaishana ni njia ya uhakika ya mafanikio katika kuzindua mipango mikuu
2023-10-18 11:27:40| cri

Ushirikiano wa kunufaishana ni njia ya uhakika ya kufanikiwa katika kuanzisha mipango mikuu ambayo inawanufaisha wote.

Hayo yamesema na rais wa China Xi Jinping leo Jumatano kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na kueleza kwamba nchi zinapokumbatia ushirikiano na kuchukua hatua kwa pamoja, pengo kubwa linaweza kugeuzwa kuwa njia ya kupita, nchi zisizo na bahari zinaweza kuunganishwa na bahari, na mahali penye maendeleo duni panaweza kugeuzwa kuwa nchi ya ustawi.

"Nchi zinazoongoza katika maendeleo ya kiuchumi zinapaswa kusaidia washirika wao ambao bado hawajafanikiwa. Sote tunapaswa kuchukuliana kama marafiki na washirika, kuheshimiana na kuungana mkono, na kusaidiana kufanikiwa," Xi alisema.

Xi aliongeza kuwa kama msemo unavyosema, "unapokaa karibu na muwaridi, lazima utanukia." Kwa maneno mengine, kusaidia wengine pia ni sawa na kujisaidia mwenyewe.

Xi alibainisha kuwa kuona maendeleo ya wengine kama tishio au kuchukulia kutegemeana kiuchumi kama hatari hakutafanya maisha ya mtu kuwa bora zaidi au kuharakisha maendeleo yake.