Juhudi za makusudi zahitajika ili kuziba pengo la kidijitali barani Afrika
2023-10-18 09:00:54| CRI

Wajumbe waliohudhuria kongamano la mawasiliano kimtandao duniani (Mobile World Congress 2023) mjini Kigali, wametoa wito kwa Afrika kuharakisha muunganisho wa kidijitali, ufikiaji rahisi na uwezo wa kumudu gharama ili kuziba pengo la kidijitali barani Afrika.

Kongamano hilo limewaleta pamoja zaidi ya wajumbe 2,500, wakiwemo viongozi wa kisiasa, serikali, wataalamu, wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, na makampuni kadhaa ya teknolojia kutoka nchi za Afrika na dunia kwa ujumla.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema teknolojia ya matumizi ya fedha kimtandao imeanza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya kila siku ya wananchi. Pia amesema uwezo wa teknolojia ya kidijitali kwenye mambo ya afya pia unaanza kubadilisha mifumo ya afya, kwa hiyo inapaswa kushughulikia mapungufu ili kufikia muunganiko kwa urahisi.