Viongozi wa nchi za nje waliokutana na Rais Xi, wazipongeza China na BRI
2023-10-18 09:01:31| CRI

Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 140 na mashirika 30 zaidi ya kimataifa wanaendelea na mkutano wa Baraza la tatu la Ushirikiano wa Kimataifa la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) unaoendelea hapa Beijing.

Jana viongozi wanane wa nchi mbalimbali walifanya mazungumzo na Rais Xi Jinping, ambapo walipongeza maendeleo ya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja” (BRI), maendeleo ya China na mchango wake mkubwa katika masuala ya kimataifa.

Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan, Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed, Rais wa Chile Gabriel Boric, Waziri Mkuu wa Hungary Bw. Victor Orban, Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Bw. James Marape, Rais wa Indonesia Bw. Joko Widodo, Rais wa Serbia Bw. Alexander Vucic, na Rais wa Uzbekistan Bw. Shavkat Mirziyoyev, kwa nyakati tofauti walifanya mazungumzo na Rais Xi, wakipongeza pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na jinsi linavyohimiza urafiki kati ya China na nchi zao.