Rais wa China asifu uhusiano wa China na Russia
2023-10-18 14:33:00| cri

Rais wa China Xi Jinping amesifu uhusiano kati ya nchi hiyo na Russia wakati alipofanya mazungumzo na rais wa Russia, Vladmir Putin siku ya Jumatano mjini Beijing.

Rais Xi amesema, uaminifu wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuimarika, na kwamba nchi hizo mbili zimedumisha uratibu wa kimkakati wa karibu na wa kufaa. Pia amesema thamani ya biashara kati ya nchi hizo imefikia kiwango cha juu katika historia na inaendelea kufikia lengo la dola za kimarekani bilioni 200 lililowekwa na pande hizo.

Kwa upande wake, rais Putin amesema Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja linatambulika kama bidhaa ya umma ya kimataifa, na ameeleza matumaini yake kuwa nchi nyingi zaidi zitajiunga na Pendekezo hilo.