Msomi wa Nigeria: “Ukanda Mmoja, Njia Moja” wasukuma mbele uendelezaji wa viwanda barani Afrika
2023-10-19 14:31:38| CRI

Natumaini u mzima buheri wa afya msikilizaji na karibu sana kwenye kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo msikilizaji, pamoja na habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, tutakuwa na ripoti inayohusu“Ukanda Mmoja, Njia Moja” wasukuma mbele kwa nguvu uendelezaji wa viwanda barani Afrika. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi kuhusu Kenya inatarajia kunufaika zaidi kutokana na ushirikiano wake na China katika ustawishaji wa miundombinu.