Bibi Peng Liyuan na wake wa viongozi wa nchi za nje watembelea Jumba la Makumbusho la Sanaa na Ufundi la China
2023-10-19 09:22:15| CRI

Mke wa Rais Xi Jinping wa China Bibi Peng Liyuan, jana asubuhi aliwaalika wake wa viongozi wa nchi za nje waliohudhuria mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kutembelea Jumba la Makumbusho la Sanaa na Ufundi la China.

Kwenye jumba hilo, Bibi Peng Liyuan na wageni wake walitazama kwa pamoja sanaa ya uchongaji wa mbao na mawe ya jade na utarizi, na pia walifahamishwa kuhusu opera za jadi za China na ala maalumu ya kale ya China iitwayo Guqin, na kufurahia maonesho ya muziki wa ala hiyo, opera za Kunqu na Beijing.

Akisisitiza kuwa utamaduni ni daraja linaloleta pamoja nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kwa umoja na ushirikiano, Bibi Peng Liyuan ameeleza matumaini yake kuwa maingiliano ya kiutamaduni yataimarishwa zaidi ili kukuza urafiki wa jadi na kutimiza maendeleo ya pamoja.